Tuesday , 13th Oct , 2015

Imeelezwa kwamba uwepo wa tuzo nyingi katika kazi za sanaa ni moja ya sababu inayoleta ushindani kwenye sanaa, ambayo huchangia kukua kwa sanaa hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Afisa habari wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Artides Kwizela, alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba lengo kubwa la utolewaji wa tuzo ni kuthamini mchango wa wasanii.

"Tuzo lengo lake kubwa ni kuthamini mchango wa wasanii ama kuna kazi wasazii wanafanya, lakini kitu cha pili tuzo zinafanya wasanii wanashindana kwa sababu kinakuwa ni kitu kina ushindani, na kwa sababu wasanii wanakuwa katika hali ya kushindana hivyo wasanii wanatengeneza kazi ambazo ni ubora ili ziweze kushindana", alisema Kwizela.

Pamoja na hayo BASATA wamewataka watu mbali mbali kujitokeza kuanzisha tuzo ili kuleta changamoto ya kufanya kazi bora kwenye sanaa.