Thursday , 26th Mar , 2015

Ikiwa kesho ndiyo siku kubwa ya mpambano wa Masumbwi wa Night of Knock-outz pale Diamond Jubilee, kutoka tasnia ya muziki wasanii wameendelea kuonesha hamasa kubwa na pia kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mpambano huo.

Msanii wa muziki wa bongofleva nchini, Tundaman

Tundaman amekuwa ni staa mwingine wa Bongofleva ambaye ametaka yeye na mashabiki wake kukutana ukumbini siku ya kesho, akiweka wazi sapoti yake kwa Bondia Thomas Mashali ambaye ni mtu wake wa karibu kutoka Manzese.

Leo hii mkutano wa kuwatambulisha mabondia watakaopambana kesho umefanyika jijini Dar es Salaam sambamba na zoezi la kupima uzito, tayari kwa mpambano wa kupasua na shoka kesho.

Kiingilio katika mpambano huo kitakuwa ni shilingi 100,000 kwa VIP na 20,000/- kwa kawaida na utapata kushuhudia burudani hiyo kali ya masumbwi sambamba na mastaa mbalimbali kutoka Tasnia ya Muziki na Bongo Movie.