Tuesday , 1st Dec , 2015

Nyota wa muziki Tunda Man, ameamua kuelimisha kundi la mama wajawazito kupitia sanaa yake ambapo mafundisho hayo yatakuwa ndani ya rekodi yake mpya ya 'Mama Kija' ambayo itatoka rasmi kesho.

Nyota wa muziki Tunda Man

Tunda Man ameeleza kuwa, kuna mambo mengi ambayo wajawazito wanapitia na kuyafanya ama kwa kufahamu au kutokufahamu, elimu ambayo itakuwa ndani ya rekodi hiyo ambayo amechukua muda wa kutosha kuitayarisha.