Thursday , 29th Jan , 2015

Msanii mwenye historia kubwa katika gemu ya muziki hapa Bongo, TID Mnyama amesema kuwa licha ya mfumo wa muziki kumkandamiza sana uwezo alionao umemsababisha kuendelea kubaki katika nafasi aliyonayo.

Msanii wa miondoko ya Bongo Fleva TID

TID amesema kuwa kwa sasa anashindwa kuelewa mfumo unataka aendeshe vipi muziki kutokana na kusahau kuwa yeye ni moja kati ya wasanii walioweza kutengeneza misingi mizuri ya wasanii wa sasa kujitengenezea faida na pesa nyingi kutokana na muziki huku wakiwa na uwezo mdogo tu.