Monday , 11th Jul , 2016

Rapa maarufu nchini Tanzania wa kundi la Weusi Nikki wa Pili amesema kwamba teknolojia ni muhimu sana katika utendaji wa kazi mbalimbali katika jamii kwani huondoa ukiritimba na kupunguza kupokea na kutoa rushwa.

Msanii wa kundi la Weusi Nikki wa Pili

Msanii huyo ameyasema hayo aliposhiriki katika kipindi cha EADRIVE kinachorushwa na kituo cha East Afrika Radio,ambapo ameshiriki kama mtangazaji mwenza katika kipindi hicho.

Akichangia mada kuhusu usafiri wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es salaam ambapo kampuni inayosimamia mradi huo UDART imetangaza kwamba inatarajia kusitisha matumizi ya tiketi za karatasi ifikapo Julai 30 mwaka huu ambapo abiria watatakiwa kutumia tiketi.

UDART wamesema Mpango huo umewalenga watu wazima ambapo kila mmoja atalazimika kutumia kadi na sio tiketi kama ilivyo sasa na wanafunzi pekee ndiyo watatumia tiketi.

Akichangia mpango huo msanii Nikki wa Pili amesema lengo hil;o ni jema na kwa nchi zinazoendelea teknolojia inasaidia sana kupunguza rushwa na ukiritimba wa kutoa huduma kwa wananchi.