
Majaji wa Dance100 2016
Akizungumza na EATV mmoja wa waratibu wa shindano hilo Bi. Bhoke Egna amewataka vijana washiriki na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika usaili wa Jumamosi kwani usaili huo ni burudani tosha ya bure kwa watu wote watakaojitokeza.
''Usaili huo kwa makundi utakuwa ni wa mwisho ambapo hatua inayofuata ni makundi 15 kuanza hatua ya robo fainali, nusu fainali, na fainali yenyewe hivyo usaili wa Jumamosi hiii pia unalenga kupata akundi matano'' Amesema Bi. Bhoke
Ameongeza kuwa kama kawaida hakuna kiiingilio katika ushiriki wa shindano hilo na vijana ambao wana umri wa miaka 18 na kuendelea wanatakiwa kujitokeza na kundi lao na kuonyesha vipaji siku hiyo na kama wakiibuka washindi wa siku wataendelea na hatua zinazofuata.