Friday , 30th Sep , 2016

Msanii mkongwe wa filamu nchini Kurwa Kikumba maarufu kama Dude ameeleza sababu za yeye kimya kwa muda katika ulimwengu wa sanaa ya uigizaji.

Dude

Akipiga story na eNewz Dude aliulizwa sababu za ukimya wake na kusema kuwa "Sanaa ya Bongo imevamiwa na watu wanaopenda pesa lakini hawana uwezo wa kufikiri, wanaotumia akili kama Diamond pekee ndiyo wanaweza kuipeleka sanaa mbali".

Dude alisema wasanii wa Bongo Movie inabidi wajilaumu wenyewe kwa kuruhusu "mtu yeyote mwenye pesa tu akiamua anaweza kuwa Producer au Director" hivyo kupelekea kazi kutoka zikiwa na kiwango kidogo.

Dude alimalizia kwa kusema inabidi kiundwe chombo cha kuratibu sanaa ya filamu ili watu wasijiamulie tu kujiingiza katika tasnia hiyo bila ya kuwa na vigezo.