Stara amesema kuwa, anakumbuka mwaka 2005 alimsaidia Mheshimiwa Sugu kufanya kiitikio katika rekodi yake, ambapo aliongozana naye studio licha ya kuwa alikuwa ndio ametoka kujifungua mtoto wake wa pili, akionelea kuwa anastahili heshima zaidi kutoka kwa mwanasiasa huyo.
Stara Thomas, nyota mkongwe wa muziki ametoa ya moyoni kuhusiana na namna ambavyo msanii na mwanasiasa maarufu sasa, Joseph Mbilinyi 'Sugu' kumuwekea kinyongo 'cha kisiasa' na kumpita bila kumsalimia,licha ya mchango wake katika tasnia ya muziki.