Saturday , 20th Dec , 2014

Staa wa muziki wa Hip Hop hapa Bongo, Stamina a.k.a Shorwebwenz amesema kuwa licha ya wasanii kubadilisha aina ya muziki wanaoufanya ili kukidhi mahitaji ya soko, yeye hatabadili mtindo wake

Stamina

Stamina a.k.a Shorwebwenz amesema kuwa, licha ya upepo wa sasa unaowasukuma wasanii kubadilisha aina ya muziki wanaoufanya ili kukidhi mahitaji ya soko,kwa upande wake hana mpango wowote wa kuhama katika upande aliopo kutokana kupenda sana na kuridhika na kile anachokifanya.

Stamina amesema kuwa, hawezi kufanya mziki mwingine wowote ule ambao haueleweki kwa lengo la kupata hela, huku akikazia kuwa katika Hip Hop tofauti na mawazo ya wengi, yeye binafsi ameridhika, na hii ikimaanisha kuwa, hata umuwekee rapa huyu fungu kubwa kiasi gani pembeni ya Hip Hop, hawezi kushawishika.