Sunday , 22nd Nov , 2015

Rapa Stamina ametolea ufafanuzi maneno makali aliyotumia dhidi ya baba yake mzazi katika rekodi yake ya Mr. Boniventure ambayo ameiachia kama zawadi ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa kwa mashabiki.

Rapa Stamina

Mkali huyo ameeleza kuwa hiyo ilikuwa ni katika kueleza hali halisi ya safari yake ya muziki, tokea kipindi cha nyuma wakati mzazi wake huyo haoni manufaa ya fani hiyo kwa mwanae.

Stamina amesema kuwa, maneno hayo yametokana na hisia alizokuwa nazo alipokuwa studio kufanya kazi hiyo, na ni kweli ni siri za binafsi za familia ikiwepo kufiwa na mama yake mzazi, akifafanua kuwa kwa sasa pia Baba yake amekuwa ni mtu wa karibu sana na rafiki ambaye anasapoti kile anachokifanya.