Friday , 29th May , 2015

Star wa muziki wa Hip Hop, Stamina ametoa kauli nzito kwa wasanii wale wanaobadilisha ama walibadilisha vionjo vya muziki wao kwa kisingizio cha kulifuata soko, hususan wale walioiacha Hip Hop kuwa ni wavamizi katika fani hiyo ya muziki.

msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Stamina

Stamina ambaye anazindua albam yake ya kwanza kabisa inayokwenda kwa jina Mount Uluguru ikiwa na nyimbo 23, amesema kuwa aina ya muziki anaofanya si wa mitindo, na kihistoria mtu mwenye uwezo wa kweli katika fani hiyo hawezi kubadilika na kufanya muziki wenye vionjo tofauti.

Star huyo amekazia kuwa lengo kubwa la muziki anaofanya ni kufikisha ujumbe na si kupata pesa, na hapa anaeleza zaidi na kuwadiss wavamizi.