Saturday , 8th Nov , 2014

Sitti Mtemvu, Mrembo aliyenyakua taji la Miss Tanzania kwa mwaka huu na kukumbana na misuko suko mbalimbali kutokana na tuhuma za kudanganya umri, leo hii amewasilisha barua rasmi ya kujivua taji hilo.

Sitti Mtemvu

Mkurugenzi wa Lino Agency yenye dhamana ya kuandaa mashindano hayo, Hashim Lundenga ameiambia eNewz kuwa, ameipokea barua ya Sitti ya kujivua taji hilo, na kwa mujibu wa taratibu zao, aliyekuwa Miss Tanzania Namba Mbili, Lilian Kamanzima ndiye atakayeendelea na taji hilo.

Sitti katika barua yake amewashukuru wale wote waliompa sapoti kutoka hatua ya awali ya mashindano haya ya urembo kutoka ngazi ya awali na kusema kuwa maneno yote yaliyosemwa juu yake yamefikia hata hatua ya kuwa tishio la usalama wa maisha yake.

Lilian kamanzima anayechukua nafasi ya Miss Tanzania