Monday , 22nd Feb , 2016

Msanii Godzila amewawakia watu wanaoshabikia masuala ya team za wasanii, na kusema kuwa unawagawa wasanii na kuua muziki.

Godzila ameyasema hayo kwenye ukurasa wake wa twitter kwa kuandika maneno ambayo ni makali, akitoa ya moyoni mwake juu ya team za wasanii.

"Tukubaliane ..mambo ya team yanaharibu mziki, waseche na team zao..tunashindwa hadi kukubali kazi sasa..sisi ni watu wa muziki", aliandika Godzila kwenye ukurasa wake wa twitter.

Katika hilo ameonekana kuungwa mkono na baadhi ya watu ambao nao hawapendi jambo hilo, linaloleta mgogoro kwa watu wengi hususan wasanii, na hiki ndicho walichokiandika. kuunga mkono suala hilo.

MeddyFox: Mie Mwenyewe Sipendi Iyo Kituuu ... King_Zillah tukubaliane ..mambo ya team yanaharibu mziki.

SHAROGANGSTAR GENIUS: MI i hate that aisee.. some few suck support tha shit

Amedeus Kizito: King_Zillah Ts true, Unajua hata nchi za jiran wanatushangaa sana. Tumeendekeza sana uteam mpaka tumesahau thamani ya mziki mzuri ni upi tena

Hayo ni maneno ya baadhi ya mashabiki ambao walikuwa wanaunga mkono kauli ya Godzill.