
Tundaman ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kueleza kuwa ilikuwa rahisi kwake mtu kumfuata akacheze mpira kuliko kumwambia waende studio kurekodi.
“Nilipokuwa naanza kuimba nilikuwa muoga sana kwenda studio tofauti na mtu akiniambia tukacheze mpira ndondo cup”, alisema Tundaman.
Tundaman aliendelea kusema kuwa sababu hiyo ya uoga ndio iliyomfanya asishiriki kuimba wimbo wa Vailet ulioimbwa na Matonya, huku yeye akiwa mwandishi wa wimbo huo.
“Vailet nimeitoa kwenye stock yangu nikaitoa nikamkabidhi mwanangu, ilitakiwa nifanye vocal lakini uoga niliokuwa nao pale studio nikamwambia Tonya malizia, nili 'change' mind tuko studio tunaingiza vocal”, alisema Tundaman.
Pamoja na hayo Tundaman amesema hakujisikia vibaya kwa hilo kwani badala yake ili kipaji chake cha kuandika kisipotee, aliendelea kuandika nyimbo na kuwapa rafiki zake waimbe, na hujisikia faraja pale anapoisikia hewani.
“Ili uandishi wangu usipotee nilikuwa naandika nikawa nampa mtu aimbe nami nikiisikia ngoma imetoka basi najisikia faraja sana “, alisema Tunda Man.
Pia Tunda Man hakuishia hapo na kuelezea changamoto walizozipitia akiwa kwenye harakati za kutoka na kusema kuwa walilazimika kutembea kwa mguu kwenda studio za Baucha zilizopo Magomeni, akiwa na producer aliyetengeneza wimbo wa Neila Maneke.
“Neila ilikuwa inafanyika magomeni studio za Baucha, Maneke ndiye kaitengeneza nilikuwa natembea nampitia Mwenbechai tunaenda studio, zoezi likawa gumu ilikuwa twende zaidi ya mara 2, wakati huo bado nacheza mpira, taratibu nikajikuta naacha kucheza, siku moja alikuja Abby Skills tukamuona mshkaji anatoa mahela kibao, nikasema duh! kumbe muziki ndo unalipa hivi na mimi nacheza ndondo cup napata kielfu 20, nikaamua kukaza mpaka hivi”, alisema Tunda Man.