Friday , 30th Oct , 2015

Msanii wa Hip Hop Stamina Sharobwenzi amesema hawezi kujilazimisha kufanya muziki asioupenda ili kufuata soko la biashara.

Stamina ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo ya east Africa Radio, na kueleza kwamba anafanya muziki waHip Hop kwa sababu anaupenda, hivyo hata kama haumlipi hatoacha kufanya.

"Mi hizi habari za muziki wa biashara sitaki hata kuzisikia, na nnakuhakikishia huwezi kuja ukanikuta mi nimebadilika nikaanza kuimba sijui vitu vitu gani, mimi nafanya Hip Hop kwa sababu ni kitu ninachokipenda kwenye roho yangu, either kinanilipa, either hakinilipi, nafanya what i feel", alisema Stamina.

Stamina aliendelea kusema kwamba si lazima mtu utoe wimbo ambao una mahadhi ya kuchezeka, kwani sio wote wanapenda kucheza muziki.

"Unasema siku hizi lazima nyimbo ichezeke, are you sure watu wote wanaenda club!? sio kila mtu anapenda kwenda club, kuna mwengine anapenda kuchil nyumbani anasikiliza nyimbo fulani hivi ambazo sio lazima zichezeke, kwa hiyo watu wanashindwa kuelewa, mi ninachohitaji ukisikiliza muziki wangu huondoki bure", alisema Stamina.