Monday , 6th Jun , 2016

Mdau mkubwa wa muziki Bongo Papaa Misifa ameibuka tena baada ya ukimya wa muda mrefu kwa kile kinachosemekana kuwa na mawazo ya kukimbiwa na baadhi ya wasanii.

Mdau wa muziki Bongo Papaa Misifa

Akizungumza na Enewz Papaa misifa alisema kuwa yeye hajaweka mikataba ya kumiliki msanii moja kwa moja kwakuwa akifanya hivyo atashindwa kukuza vipaji wa wasanii wengine wachanga wakati kazi yake ni kunyanyua vipaji vya wasanii mbalimbali viendelee kusonga mbele.

“Mimi ni mtu wa kutoa vipaji vilivyokuwa chini visivyojulikana nivifikishe mbali halafu niviache kuna watu wengine wachukue waendelee nao hapa kwahiyo ukiona msanii sipo nae tena haina maana kanikimbia nimeona amefika mbali nawaachia na wengine waendelee nae”,alisema Papaa misifa.

Pedeshee huyo ambae ameshawahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali akiwemo Diamond, Rich Mavoko,Dayna Nyange na wengine wengi amezindua studio yake jana na kudai kuwa amejipanga kuwaondoa hofu wale wote ambao walikuwa wanajua wasanii wengine wa chini hawawezi kufanya vizuri katika game ya muziki na kuongezea kuwa kila msanii atakaeenda kufanya kazi na yeye basi akifikisha uwezo wa kuweza kutangaza nchi yake anamuachia na kuchukua mwingine.