Sunday , 19th Apr , 2015

Mwimbaji nyota wa nyimbo za injili nchini Tanzania Christina Shusho anajianda kufanya ziara kubwa ya muziki nje ya nchi zitakazoanza kuanzia mwezi wa tano, wa sita hadi wa saba mwaka huu akianzia nchi ya Marekani, Canada na Uingereza.

mwimbaji wa muziki wa injili nchini Christina Shusho

Kutokana na maswala ya uchaguzi mkuu nchini kuonekana kuchukua nafasi kubwa katika programu zake, mwimbaji huyo ameelezea kuwa hivi sasa anajiandaa kutoa video ya wimbo unaobeba jina la albamu yake mpya iliyopo hivi sasa sokoni inayoitwa'Ongoza hatua zangu'.