
Manfongo na Silole
Manfogo ameiambia E news kwamba hakumshirikisha shilole katika video yake ili kuuwa winbo wa chura kama watu wanavyoongea bali yeye alimpigia simu mwana dada shishi na kumuomba amtafutie video queen wa wimbo huo ndo shishi akasema nitamaliza mwenyewe (kwa maana kwamba yeye mwenyewe atakuwa video qeen)
Ameendelea kusema "Singeli sio muziki wa kihuni kama watu wanavyodhani ila ni muziki ambao umetokea kupendwa na wadada wengi ndo maana unaonekana ni wa kihuni, lakini singeli ni muziki wenye nguvu sana katika sanaa na unakuja kwa kasi sana."
Hivyo amewaahidi mashabiki wake kwamba kazi nyingi zinakuja na wategemee kuona video katika kila wimbo atakao utoa kwa sasa.