Baba Levo
Baba Levo aliyasema hayo alipofanya mahojiano na kipindi cha eNewz cha East Africa Television, na kusema kuwa mambo anayoyafanya Shilole yanamlazimu akae mbali naye, ili kujiepusha na lawama.
“Shilole kuna baadhi ya vitu ananiudhi, sasa hivi ana nguvu kubwa na umaarufu mkubwa kwenye mikoa wa kufanya show na kuingiza hela nyingi, kwa hiyo mimi nilikuwa nataka tutumie hiyo timing kutengeneza pesa, kama marafiki ye akitengeneza pesa na mimi nitapata pia, lakini unaona anajifanyia vitu kama uhanangwa uhanangwa, mara kafanya hivi mara hivi, sasa ili usigombane naye unakaa mbali naye, kama unamshauri mtu kitu hafuati huo ni uhanangwa”, alisema Baba Levo.
Baba Levo aliendelea kusema kuwa tabia ya msanii huyo ya kubadilisha wanaume kila siku kwake haina tatizo kwani Shilole ni msichana mrembo hivyo ana kila sababu ya kupendwa na kuchagua maisha yake.
“Shilole ni msichana mzuri, ukitoka wewe ukajifanya humtaki anakuja mwingine anampenda sana, ni maisha amejichagulia anataka kuishi kama Lady Gaga, hata kama alikuwa anafanya mambo ya kihanangwa ni kuweka mambo yake hadharani”, alisema Baba Levo, anapoweka mambo yake mitandaoni si kitu kizuri".