mtayarishaji wa muziki nchini Sheddy Clever
Sheddy ameweka wazi kuwa, kazi hii imekuwa ni kubwa na imemgharimu kiasi kikubwa cha pesa ambacho hakuwa tayari kukitaja na kusema kuwa, bado kazi ya kuweka sawa studio hiii inaendelea.
Mtayarishaji muziki huyu ameiambia eNewz kuwa, licha ya kufungua rasmi studio wiki hii, kuna vifaa bado vipo njiani kuletwa na baada ya wiki mbili kazi ya kufunga na kuweka mambo sawa itakuwa imekamilika kabisa.
Sheddy amesema kuwa, kazi hii ni matunda ya mafanikio ya kazi ambazo amekuwa akifanya na kukanusha kuwa na mtu nyuma yake ambaye ameweka mkono kufanikisha shughuli hii.