Thursday , 3rd Apr , 2014

Shappaman, staa wa muziki wa nchini Kenya ambaye aliibuka katika umaarufu akiwa anafanya kazi pamoja na kundi la Camp Mulla ambalo mpaka sasa limegawanyika, ameweka wazi sababu halisi ya kufikia kikomo kwa kundi hilo.

Camp Mulla wakati wapo pamoja

Shappaman ameweka wazi kuwa, mgawanyiko wa kundi hilo ulikuwa hauna budi kutokana na wanakikundi Thee MC Africa maarufu kama Taio na Lady Karun ama Miss Karun kutakiwa kuwa katika ratiba nyingine nje ya nchi, kitu ambacho kilileta kikwazo kikubwa kwa wao kuendelea kama kundi.

Maelezo haya ya Shappaman yamekuja baada ya kuwepo kwa maswali mengi juu ya sababu hasa ambayo ilisababisha kundi hili kuizima nyota yao mara tu baada ya kuingia katika jukwaa la kimataifa la muziki.