Thursday , 21st May , 2015

Kundi la muziki la Sauti Sol kutoka nchini Kenya, limejipanga kwa ajili ya kuanza ziara yao nchini Marekani kwa siku kumi kuanzia leo, ambapo watafanya maonesho zaidi ya matano nchini humo.

wasanii wa kundi la muziki la Sauti sol nchini Kenya

Kundi hilo ambalo linajivunia mafanikio makubwa ya kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa za muziki za kimataifa kutoka nchini humo, linatarajiwa kupata mapokezi makubwa na kutumbuiza Minneapolis, Washington DC, Dallas TX na North Atlanta, GA.

Ziara ya kundi hilo nchini humo inatarajiwa kufanya kazi kubwa ya kutangaza ladha ya muziki kutoka Afrika Mashariki, kuwatangaza zaidi kama kundi kimataifa na kukuza wigo wa mashabiki wao katika nchi hiyo iliyoendelea kiburudani.