Thursday , 2nd Apr , 2015

Prodyuza mahiri wa miondoko ya Bongo Flava nchini, Sappy ambaye hivi sasa makazi yake yapo nchini Kenya amewasapoti wasanii kufanya kolabo na wasanii wa nje ya nchi kutokana na kile ambacho anasema ni kujijengea kujiamini katika soko hilo.

Prodyuza wa miondoko ya Bongofleva nchini Herry Sappy

Sappy ambaye amefanya kazi na mkali Redsan, amesema kuwa zoezi hili tayari limeonekana kwa wasanii wengi nchini ambao hivi sasa wanazidi kuliteka soko la Afrika na hivi ndivyo prodyuza huyo alivyofunguka kupitia enewz.