Friday , 16th Oct , 2015

Meneja Said fella au Mkubwa na wanawe amesema kuwa kutokana na siku chache zilizobakia kuelekea uchaguzi mkuu tarehe 25 mwezi huu, amewasihi watanzania kuweka amani mbele na kuelezea kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.

Meneja Said fella almaarufu kama Mkubwa na wanawe

Said Fella ambaye ni mgombea wa nafasi ya udiwani wa kata ya Kilungule ambaye hivi sasa ameweka makazi yake huko, ameiambia enewz kuwa ni muhimu kuilinda amani kwani yawapasa watanzania wote kuweka kando suala la itikadi ya vyama pinzani huku akiwasihi watanzania wote kupiga kura kwa amani na utulivu.