Sunday , 4th Nov , 2018

Msanii wa Bongo Fleva, Ruby ameibuka na kujibu tetesi zinazomuhusisha yeye kuwa na ujauzito kutokana na mabadiliko yanayoonekana katika mwili wake hivi sasa.

Ruby na mpenzi wake mpya

Msanii huyo ambaye hivi sasa anatamba na wimbo wa 'Ntade' amesema kuwa suala la yeye kuwa na ujauzito ni la kawaida na kama itakuwa ni kweli basi itaonekana.

Akizungumza katika FNL ya EATV, Ruby amesema, "nadhani ujauzito ni baraka lakini pia sio kitu cha kuficha kwasababu mwisho wa siku kinaonekana, kwahiyo mwenye macho haambiwi tazama".

Alipoambiwa kuwa mashabiki wake ndiyo wanaosema kuwa tumbo lake linaongezeka, Ruby alimalizia kwa kusema "Ahsante".

Ruby pia amemtambulisha mpenzi wake mpya anayejulikana kwa jina la 'Kusa' ambaye ni mwanamuziki na mwandishi wa nyimbo.

Kwa mujibu wa Kusa, mapenzi yao yana muda wa mwaka mmoja sasa na kwamba wameona ni wakati wa kuonekana hadharani kwakuwa tayari wameshatambulishana kwa wazazi wao.