Nyota wa muziki Kenya Ringtone
Ili kufikisha ujumbe wake Ringtone ameshirikiana na umati wa wasanii ambao walifanya maandamano wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kumtaka Okoth kung'oka, sambamba na kutaka kuongezeka kwa asilimia za mgao wa mirahaba kwa wasanii.
Hatua hii inakuja ikiwa ni wiki tu imepita baada ya msanii huyo kupatiwa barua na wanasheria wa mamlaka hiyo kumzuia baada ya kutoa tishio la kumuanika mkuu wa mamlaka hiyo kutokana na tuhuma za utendaji mbovu.