Tuesday , 13th Oct , 2015

Nyota wa muziki Wizkid ambaye anatarajiwa kutua Dar kwaajili ya onesho kubwa kabisa la Wizkid Live in Dar tarehe 31 mwezi huu, anaweka rekodi ya kuwa nyota kutoka Afrika ambaye amekwishachaguliwa kuwania tuzo kubwa zenye hadhi ya kimataifa.

Nyota wa muziki wa nchini Nigeria Wizkid

Rekodi hiyo kutoka kwa nyota huyo ameweza kuchaguliwa mara 64 ndani ya miaka 5 ambaye amekuwa akifanya vizuri zaidi katika game barani Afrika na kimataifa.

Staa huyo ambaye kwa sasa yupo huko London akimalizia Mixtape yake ya #SFTOS kati ya shughuli nyingine za shoo, pia anashikilia rekodi ya kuwa staa ambaye amekwishafanya kazi na wasanii wengi na wakubwa zaidi kimataifa, akiwepo Drake, Rihanna, Tyga na Chris Brown kati ya wengine.

Star huyo ambaye anaongoza kwa kuwa na Hit Songs Nyingi zaidi, anaamsha hamasa na joto la furaha kwa mashabiki wake Afrika Mashariki ambapo kwa kushirikiana na King Solomon Entertainment, East Africa Television na East Africa Radio wamechukua hatua ya kuwaletea Live mkali huyu.

Kumbuka ni #WizkidLiveInDar tarehe 31 mwezi huu ndani ya viwanja vya Leaders Club.