Philip Mangula akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya Hagafilo mkoani Njombe wakati akitoa ufafanuzi wa katiba Pendekezwa.
Akizungumza na wanafunzi wa sekondari, chuo na walimu katika shule ya Hagafilo Mkoani Njombe wakati akitoa elimu ya katiba pendekezwa, amesema kuwa ameisoma katiba yote na hajaona kipengele kinacho zungumzia masuala ya udini wala mahakama ya kadhi.
Lakini hata hivyo viongozi wa dini wanapinga muswada wa mahakama ya kadhi kupitishwa bungeni na kuwa sheria.
Amesema kuwa alikuwa katika kanisa moja anako Sali mchungaji wake alisema kuwa waumini wasiipigie kura katiba pendekezwa kwa kuwa ina masuala ya Mahakama ya Kadhi alipo muuliza ni katika kipengele gani kinacho zungumzia mahakama hiyo mchungaji huyo hata kipengele hicho alisema hakifahamu.
Amesema kuwa katiba hiyo haina kipengele hata kimoja kinachozungumzia dini yoyote na kuna kipengele kinacho zungumzia utawala wa sheria na kuwapo kwa mahakama huru
Amesema kuwa katika katiba pendekezwa kuna misingi ya utawala bora na umiliki wa ardhi na kuwa ardhi hiyo inatunza na kuwa ni mali ya mtanzania wa kizazi cha sasa na cha baadaye.
Katika hatua nyingine Mangula ameungana na kauli ya kiongozi katoriki Muadhama Kadinali Policarp Pengo kuhusiana na kuwaruhusu wananchi kuchukua maamuzi yao wenyewe juu ya kupiga kura ya ndio au hapana.
Amesema kuwa wananchi wakiisoma katiba wao wenyewe wakaielewa kama kuna mapungufu watayaona waikatae wao wenyewe na wanaosema isipigiwe kura wawe na hoja kwanini isipigiwe kura na sio wanasema hivyo bila kuwa na hoja sahihi.