Wednesday , 2nd Jul , 2014

Rapa wa siku nyingi wa nchini Kenya Jimwat aliyepotea katika gemu baada ya kuathirika na matumizi ya mihadharati na kisha kukumbwa na maswahibu ya kupata ajali mwezi Oktoba mwaka jana, hivi sasa anajiandaa na ujio wake mpya.

Rapa Jimwat wa nchini Kenya

Taarifa kupitia swahiba wake ambaye ni msanii, Dj na mtayarishaji wa muziki Madtraxx, ameelezea kupitia mtandao wa twitter kuwa tayari wamekwisharekodi baadhi ya nyimbo japokuwa hakupenda kuelezea zaidi kuhusiana na kazi hizo mpya.

Rapa Jimwat amekuwa akipitia katika misukosuko mingi ikiwemo ya ulevi wa pombe kupindukia lakini amekuwa akisapotiwa sana na watu wake wa karibu ambapo sasa mashabiki wanasubiria ujio wake huo mpya.