Thursday , 26th Feb , 2015

Radio na Weasel, mastaa wa muziki kutoka nchini Uganda wamefanikiwa kushinda tuzo ya Honesty Oscar katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kiharakati kutokana na wimbo wao kuvutia wengi na kubeba ujumbe mzito kupinga masuala ya rushwa.

Radio na Weasel

Mastaa katika kipengele hiki wamekabiliana na ushindani mkali kutoka kwa wasanii kama Juliani kutoka Kenya, Takun J, na vilevile Latgram miongoni mwa wengineo kadhaa.

Tuzo hizo zinazoandaliwa na shirika la One na Honesty Lab zimeandaliwa kwa lengo la kutambua wanaharakati mbalimbali katika kampeni yao kubwa ya kutokomeza rushwa duniani.