Tuesday , 27th May , 2014

Msanii wa muziki Moze Radio pamoja na Pallaso, wamegonga kwa kasi vichwa vya habari nchini Uganda, baada ya kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi kwa nyakati tofauti baada ya wawili hawa kuingia katika ugomvi na kupigana.

Chanzo cha Ugomvi wa Radio na Pallaso ni kauli ya mshkaji mmoja kutoka kundi la Mose kumwambia AK47 kuwa ndugu yake wa damu, Pallaso anatakiwa kumuheshimu sana Moze Radio kutokana na yeye kuwa ndiye aliyemtoa kimuziki, kauli ambayo haikumfurahisha AK47 hata kidogo.

Kwa mujibu wa ripoti, baada ya kauli hii Pallaso alipigiwa simu kufika eneo la tukio ambapo alianzisha ugomvi mkubwa uliovutia wana usalama kuingilia kati ili kuweka mambo sawa.