Friday , 28th Mar , 2014

Kesi ya mauaji inayomkabili nyota wa mbio za olympiki za walemavu, Oscar Pistorious inayoendelea
huko Afrika Kusini, imefikia hatua nyeti ya upande wa utetezi kutoa ushahidi wake.

Oscar Pistorious

Pistorious mwenyewe akiwa kama shahidi namba moja, atakuwa akijitahidi katika kuishawishi mahakama kuwa hakumuua mpenzi wake Reeva Steedcamp kwa kukusudia.

Oscar akisaidiwa na mwanasheria wake wanatarajiwa kutoa maelezo ambayo yatamshawishi jaji
anayesikiliza kesi hiyo kuwa hakuuwa kwa kukusudia, huku akiwa anabanwa na ushahidi kutoka kwa
jirani zake kuwa siku ya tukio kulisikika sauti za yowe kabla ya risasi kuashiria kuwa Orcar
aligombana na Reeva kabla ya kumpiga risasi.

Swala jingine ambali linambana Oscar ni sheria za umiliki wa silaha za moto Afrika Kusini,
ambazo zinamtaka mmiliki aliyeidhinishwa kutokutumia bunduki yake isipokuwa tu pale mazingira
yanapolazimu sana kutumia silaha hiyo ili kujiokoa katika hatari.