Saturday , 25th Oct , 2014

Msanii mkubwa wa filamu, Rn Perlman ambaye amepata nafasi ya kuitembelea Kenya katika ziara yake kubwa Afrika, ameweka wazi namna anavyomkubali staa wa filamu Lupita Nyong'o kutokana na uhalisia wake ambao umemfanya kupokelewa vizuri katika filamu.

Ron Perlman

Perlman amesema kuwa, alipata nafasi ya kukutana na Lupita na kugundua kuwa ni mrembo ambaye ni rahisi kwa kila mtu kumpenda, na kila mmoja anafurahia mafanikio makubwa ambayo amejipatia kutoka fani ya uigizaji.

Mwigizaji huyu katika kumbukumbu zake pia, miaka 34 iliyopita alikwishafanya kazi ya kupiga picha za filamu ya Quest For Fire ambayo ilifanyika katika hifadhi ya Tsavo huko nchini Kenya.