Wednesday , 27th Jan , 2016

Miezi kadhaa toka staa wa muziki Aslay kutoka Yamoto Band kutangaza mahusiano yake wazi, akimuanika hadharani mrembo Kaisi kuwa ndiye anayeushika moyo wake, nyota huyo sasa ameweka tena hadharani kuwa kwa sasa hayupo katika mahusiano yoyote.

Aslay

Hatua hii inakuja baada ya eNewz kupata za chini ya kapeti kuwa Aslay amempachika ujauzito mrembo huyo na kumuweka kando suala ambalo amekataa kulithibitisha wala kulikanusha akidai kuwa kwa sasa hayupo katika mahusiano ya aina yoyote.

Aslay ameeleza kuwa, kuhusiana na kinachoendelea katika upande wa mahusiano yake ya kimapenzi kwa sasa, atafutwe siku nyingine kukizungumzia, akiwa sasa hata katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, picha zake na aliyekuwa mwenzi wake hazionekani tena.

#DingiMtoto