Wednesday , 13th May , 2015

Msanii Chin Beez amesema kuwa shughuli ya upigaji picha za ngoma yake ya 'Pakaza' aliyomshirikisha G Nako, ilichelewa kutokana na muongozaji Hanscana na pia G.Nako kuwa na shughuli nyingine nje ya mkoa.

wasanii wa Bongofleva Chin Bees na G Nako

Mkali huyo ameongea na Enewz akisema kuwa yu mbioni kuanza kazi hiyo ndani ya wiki hizi mbili baada ya watu hao muhimu kwa kazi hiyo kurejea na mipango imeshakaa sawa, ikiwepo sehemu ya kufanyia video hiyo na hapa anaeleza zaidi.