Wednesday , 4th Mar , 2015

Kundi la muziki la Pah One, ambalo limeweza kupotea katika gemu ya muziki kwa muda mrefu sasa, limesema kuwa ukimya wao ulitokana na shughuli zao za muziki ambazo zilikua zinaendelea huko Congo, Ivory Coast na Afrika Kusini.

wasanii wa kundi maarufu la Pah One nchini Tanzania

Pah One wamerejea na rekodi inayoitwa Kizubaneta ambayo ni maalum kwa ajili ya kuwashangaza mashabiki wao.

Ola kutoka Pah One amesema kuwa, mdundo wa rekodi hiyo umefanyika huko Ivory Coast na video kufanyika Afrika Kusini, wakiwa na toleo maalum la Tanzania ambalo ndilo linaloonekana hapa, na hapa Ola anaeleza juu ya mchakato huo mzima wa rekodi hii.