Thursday , 27th Feb , 2014

Kundi la muziki la P Unit la nchini Kenya, limetajwa kuwa ndio kundi maarufu zaidi la muziki lililoteka vituo vya radio vya nchini humo, ambapo wanaongoza kwa kipato kinachotokana na mauzo na matumizi ya kazi zao katika media.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa mamlaka ya Hakimiliki za Muziki huko Kenya, MCSK ambao wameweza kuhakikisha kuwa wasanii wa Kenya wanavuna kila wanachostahili kutokana na kazi zao za sanaa.

Kwa rekodi hii, P Unit ambao kwa sasa wanatamba na ngoma yao mpya ya L.O.V.E wanasimama katika nafasi muhimu kabisa ya kusherekea mafanikio ya muziki wao, na vile vile kupata changamoto ya kutengeneza kazi nzuri zaidi ili kuendelea kushika nafasi hii ambayo ina ushindani mkubwa.