Monday , 28th Jul , 2014

Mtayarishaji mkali wa muziki Bongo, P Funk Majani katika mpango wake wa kusaka wasanii ambao atawasaini chini ya lebo ya Bongo Records tayari kwa ujio mpya, amesema amefurahishwa kusikia vipaji vingi vipya katika sanaa ya muziki kwa sasa.

mtayarishaji wa muziki nchini P Funk majani

Katika zoezi hili ambalo analiendesha kwa njia ya mtandao kwa kutumiwa Demo, P Funk ameweka wazi kupokea zaidi ya demo 100 za wasanii, huku akikosa kuona muamko kutoka kwa wasanii wa kike ambao amewataka nao kushiriki katika nafasi hii.

Zoezi hili linatarajiwa kuwa na matunda mazuri katika kuibua vipaji vingi vilivyopo mtaani na kuviingiza katika soko la muziki ambalo limekuwa kwa kiasi kikubwa katika miaka ya karibuni.