
One amefunguka hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusema siku zote namba moja yake kwa wasanii anaowakubali katika muziki wa Hip hop huwa inapiganiwa na Fid Q pamoja na Hashim Dogo.
"Siku zote namba moja yangu huwa inapiganiwa sana na Fid Q na Hashim Dogo, mimi mwenyewe huwa wananichanganya hapo lakini wasanii wengine nao wakubali ni pamoja na Prof Jay, Nikki Mbishi pamoja na mimi mwenyewe" alisema One The Credible.
Mbali na hilo rapa huyo alisema anamkubali pia Nash MC lakini hayupo katika list ya wasanii watano ambao anawakubali yeye.