Thursday , 26th Nov , 2015

Rapa Octopizzo kutoka nchini Kenya, hatimaye amezungumzia juu ya uhasama ulioanzishwa na staa wa muziki Juliani juu ya ni nani mfalme wa rap Kenya, kati yake rapa Khaligraph pia Rabbit, na kusema kuwa hatajibu lolote katika ligi hiyo.

Rapa Octopizzo kutoka nchini Kenya

Octopizzo amesema kuwa anaichukulia kama kitu cha kupoteza muda tu licha ya mashabiki kupokea ligi hiyo kwa uzito wake, binafsi anachukulia kama kiki tu ambayo itapita, akikataa kujihusisha nayo kutokana na ukweli kuwa hakuna pesa wala faida yoyote ambayo yeye kama rapa mjasiriamali atajivunia ndani yake.

Kufuatia kauli hiyo, hakuna majibu yoyote mpaka sasa kutoka kwa wasanii ambao wanatajwa ndani yake, ikikumbukwa pia kuwa Nameless alitoa kauli hivi karibuni kuwa, anasubiri kukabiliwa na wasanii hao wanaotajwa kuwania ufalme wa Rap Kenya mara baada ya kumaliza mchezo wanaofanya wa kugombania taji hilo.