Monday , 30th Jun , 2014

Nyota ya rapa kutoka Kenya, Octopizzo imeendelea kung'ara kwa upande wa kimataifa, ambapo mbali ya mafanikio katika muziki na biashara zake, ukurasa wa msanii huyu katika mtandao wa Facebook umeweza kuhakikiwa ama kuwa "verified".

Rapa Octopizzo wa nchini Kenya

Hatua hii ya kuhakikiwa kwa ukurasa wa msanii huyu, inakuwa ni nafasi nyingine nzuri kuwasaidia mashabiki wake kutokupata tabu ya kutofautisha kati ya Octopizzo wa ukweli na wale matapeli katika njia hii muhimu ya mawasiliano.

Sambamba na hili, rapa huyu pia katika orodha ya mafanikio yake kimataifa, ameweza kutambulisha shughuli zake nje ya mipaka ya Kenya, na hivi karibuni kufanyiwa mahojiano na kituo kikubwa kabisa cha habari cha kimataifa.