Friday , 12th Jun , 2015

Nyota Ndogo, msanii wa muziki wa nchini Kenya amemshambulia tena kwa maneno makali mtandaoni Colonel Moustapha ambaye ni hasimu wake, akitaka msanii huyo ahasiwe.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Nyota Ndogo

Kuhasiwa kwake kwa Mustapha unakuja sambamba na maoni kuwa wanaume wote wanaowaumiza wake zao, wanapaswa kufanyiwa hivyo.

Katika ujumbe wake huo, Nyota Ndogo akishirikiana na mashabiki zake, wametoa pendekezo kuwa msanii huyo anafaa kupelekwa huko Nyeri kwa ajili ya kufanyiwa mchakato huo, ambapo mpaka sasa Moustapha mwenyewe ajajibu mapigo.

Hii inakuwa si mara ya kwanza kwa Nyota Ndogo kumshambulia msanii huyo, akiweka wazi kuchukizwa kwake na tabia ya staa huyo kuwadhalilisha na kuwatumia wanawake vibaya katika sanaa yake.