Saturday , 17th May , 2014

Nyota Ndogo, staa wa muziki kutoka nchini Kenya ameamua kutumia vizuri nafasi yake kama msanii kwa kutoa ngoma mpya ambayo inazungumzia uhalisia wa matatizo makubwa yanayoikumba jamii kama matumizi mabaya ya pombe, dawa za kulevya na ngono.

Nyota Ndogo

Msanii huyu ameweka wazi kuwa, rekodi hii ilikuwepo katika hifadhi ya kazi zake na hakuwa na mpango wa kuitoa mpaka alipoona kuwa, changamoto alizoimba juu yake zinaisumbua jamii kwa kiasi kikubwa katika wakati huu.

Nyota Ndogo kwa muda sasa ameonesha namna ambavyo amekuwa akiguswa na matatizo mbalimbali yanayokabili jamii inayomzunguka na kutumia usanii wake kuyazungumzia kwa lengo la kuchangia katika kuleta mabadiliko.