
Kauli hiyo ya BASATA imetolewa na Mkuu wa matukio wa Baraza la Sanaa Taifa alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari kwenye studio za East Africa Radio, na kusema kwamba asidhani kufanya muziki wa nje ndio kuwa na soko.
“Huyo anayesema kitu kama hicho ana mawazo mfu, ninasema ana mawazo mfu kwa sababu ni limbukeni anataka kuiga kitu kisicho cha kwake kwa hiyo mi namwita limbukeni” alisema Maregesi.
Bwana Maregesi aliendelea kwa kusema kwamba kuiga muziki wa nje sio kuweza kupata soko, isipokuwa ni ukosefu wa elimu ya sanaa.
“Asidhani kufanya muziki wa Marekani au wa Uingereza, au wa Nigeria ndiko kuwa na soko, utakuwa na soko la wapi!? Kwa sababu huwezi ukapiga muziki kuliko huyo mwenye chake, la tatu shida tuliyonayo ya wasanii wengi wa Tanzania tunafanya kazi ya sanaa bila kusomea”, aliendelea kusema Maregesi.
Pia Bwana Maregesi amewataka wasanii kuthamini kazi za nyumbani na kujikita zaidi kufanya muziki wenye asili ya Tanzania, kwani ndio utakaowapa soko kimataifa kwa utanzania wao.