Thursday , 10th Nov , 2016

East Africa Television LTD imeendelea kutaja 'nominees' wa vipengele vingine viwili watakaowania EATV AWARDS.

Ibrahim kutoka Vodacom (Kushoto) akiwa Dullah katika Planet Bongo iliyoruka LIVE kutoka Mabibo Hostel, akitangaza majina ya wasanii walioingia katika Tuzo za EATV

Kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio, EATV LTD ikishirikana na Vodacom Tanzania na CocaCola imetaja vipengele viwili vya kundi bora la mwaka, na video bora ya mwaka, ambapo wasanii kutoka nchi 3 za Afrika Mashariki, wamefanikiwa kupenya.

Wasanii hao tukianzia na kundi bora la mwaka ni:

Navy Kenzo – 'Kamatia chini' 

Mashauzi Classic – 'Kismet '

Wakali wao - 'Chozi langu utalilipa' 

Team Mistari – 'Tuzidi' (Kenya)

Saut Sol – 'Unconditional bae' (Kenya)

Kipengele cha pili ambacho 'nominees' wake wametangazwa leo ni kundi la video bora ya mwaka, ambapo video zilizoingia ni:

Njogereza – Navio (Uganda)

Don't bother – Joh Makini 

Namjua - Shetta

Aje – Alikiba 

NdiNdiNdi – Lady Jaydee

Vipengele vingine vitaendela kutajwa siku ya Ijumaa ya tarehe 11 Novemba, na kuhitimisha zoezi hilo.

EATV AWARDS zinatarajiwa kufikia kilele chake tar 10 Desemba 2016, ambapo zitahusisha wasanii wa muziki na filamu wa nchi za Afrika Mashariki.

Tags: