Wednesday , 22nd Jun , 2016

Msanii wa kike Naj ambaye ni mpenzi wa Baraka Da Prince amerudi kutoka UK na mtu mzima Baraka alienda kumpokea viwanja vya Mwalim JK.

NAJ

Enewz ilipata nafasi ya kupiga naye story na kutaka kujua ni ishu gani huko UK anayoifanya.......

Naj alisema kule UK anafanya biashara ya kupangisha watu nyumba yaani yeye anachukua nyumba nyingi na kuwapangishia watu nyumba hizo, ni biashara ambayo Naj anasema inamlipa kinoma noma na kumfanya maisha yake yaende poa.

Hata hivyo Naj ameendelea kuiambia Enews kwamba ana ndoto za kufunga ndoa na mpenzi wake wa sasa Baraka,hivyo wapenzi wao waendelee kuwaombea mema na baraka katika mahusiano yao ili waweze kufika mbali.

Pia Naj amesema yeye kwa sasa hasomi tena mbali ana dili na ishu za movie, uimbaji na biashara mbalimbali akiwembo hizo za kupangishia watu nyumba UK na biashara nyingine hapa hapa nchini.