Wednesday , 5th Aug , 2015

Staa wa muziki wa nchini Uganda, Eddy Kenzo ameendelea kupata mashavu kupitia rekodi yake ya “Sitya Loss” kimataifa, baada ya watayarishaji wa filamu kubwa huko Afrika Kusini kuwasiliana naye wakitaka kutumia rekodi hiyo katika filamu yao.

Staa wa muziki wa nchini Uganda Eddy Kenzo

Shavu la kutumia kazi hiyo katika filamu, litamuongezea zaidi staa huyo nafasi ya kuwafikia mashabiki wengi zaidi na wa aina tofauti, ikielezwa pia kuwa stahiki zote zitarejeshwa kwa msanii huyo kulingana na matumizi ya kazi yenyewe.

Filamu hiyo inatayarishwa na shirika la utangazaji la huko Afrika Kusini na tayari imewekwa wazi kuwa itasimama kwa jina la ‘The Native’.