Tuesday , 19th May , 2015

Staa wa muziki kutoka Kenya, Nazizi ambaye kwa sasa yupo hapa Bongo ameieleza eNewz kuwa ujio wake nchini safari hii ni kwa ajili ya kukamilisha na kutangaza albam ya kundi jipya aliyoifanya na More Fire, kukiwa na project za kutanguliza za kuachia.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Nazizi

Nazizi amesema pia kuwa sambamba na kazi hiyo ana video ambayo ameifanya na Director Hanscana wa hapa Bongo ambayo, ziara hii ni kwa ajili ya kuiachia kama anavyoeleza mwenyewe hapa.

Pembeni ya hilo, staa huyo mkongwe katika game akawataja producers wakali ambao anawakubali zaidi hapa Bongo, akiwepo P Funk, Lamar na Dunga katika nafasi za juu za orodha yake, sambamba na kushukuru kituo cha EATV kwa sapoti katika muziki wake.