Wednesday , 2nd Dec , 2015

Nyota wa muziki Naj ameeleza kuwa, hatua kubwa ambayo muziki wa hapa nyumbani umepiga, umetoa nafasi zaidi kwa wasanii wa aina yake kuchanganya ladha zaidi na kukubalika sana na mashabiki wa muziki wake.

Nyota wa muziki nchini Tanzania Naj

Hii inakuwa tofauti na hapo awali ambapo mtindo aliokuwa akiufanya Naj ulikuwa ukikosolewa kwa kuhusisha sna uzungu.

Naj amesema kuwa, kutokana na muziki kuingia katika anga la kimataifa anajisikia huru zaidi na kupokelewa na mashabiki wa aina tofauti, akiwa sasa amerejea na project yake kubwa, 'No Going Home'.

Naj pia akaeleza siri ya kufanya vizuri katika muziki wake sasa, kuwekeza pesa za kutosha kitu ambacho hajutii kukifanya, akiwa pia na kolabo kubwa kabisa akiwa na Jose Chameleone ambayo anaiweka hapa.