Monday , 15th Dec , 2014

Mwanamuziki nyota wa Taarab nchini Tanzania, Mzee Yusuf maarufu kama mfalme wa taarab, amesema wimbo wake mpya wa 'Mahaba Niue', utakuwa wa mwisho kwake kutoa kabla ya kupumzika kabisa kutoa nyimbo mpya.

mwimbaji nyota wa taarab nchini Mzee Yusuf

Akiongea kwenye kipindi cha Tam Tam za Mwambao cha East Africa Radio, Mzee Yusuf amesema wimbo huo utakaokuwa ni zawadi pekee kwa mashabiki wake wa taarab utatoka hivi karibuni.

Amesema baada ya kutoa wimbo huo, ataacha kabisa kutoa nyimbo mpya, na badala yake atakuwa anawatungia nyimbo waimbaji wake, na yeye atakuwa akipanda kuimba nyimbo zake za zamani tu.